Buhari atoa ndege mbili kwa jeshi la Nigeria

Ndege mbili zimetolewa kwa jeshi la wanahewa la Nigeria Haki miliki ya picha Nigeria Government
Image caption Ndege mbili zimetolewa kwa jeshi la wanahewa la Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa ndege mbili kutoka kwa ndege za rais kwa jeshi la wanahewa la nchi hiyo

Msemaji wa raia alichapisha picha za kutolewa kwa ndege hizo kwenye mtandao wa Facebook.

Wiki iliyopita msemaji wa rais Garba Shehu alisema kuwa wataweka tangazo kwenye magazeti kutafuta wanunuzi wa ndege zingine mbii za rais.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kwa sasa Buhari ana jumla ya ndege sita

Hatua hiyo inapunguza idadi ya ndege za rais hadi 6 sita kutoka ndege 10.

Hii ni moja ya hatua ya kupunguza matumizi yasiyohitajika.