Hull city yamtangaza Phelan kuwa kocha mkuu

hull city Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mike Phelan kocha wa Hull city

Klabu ya soka ya Hull City, imemtangaza Kocha wa muda wa timu hiyo Mike Phelan, kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Phelan amekua kocha wa muda wa Hull City ama Chui wa njano, toka aliyekua kocha mkuu Steve Bruce, kubwaga manyanga.

hata hivyo huenda timu hiyo ikawapoteza kocha msaidizi Stephen Clemence, na mlinda mlango Gary Walsh, ambao kocha wa zamani wa timu hiyo Steve Bruce, anawataka kwenda kujiunga nae katika klabu yake mpya ya Aston Villa.

Mwanzo mzuri katika ligi kuu ya England kwa kocha huyu kulimfanya kuwa kocha bora wa mwezi wa Nane.

Hull city,wako katika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi wakiwa wamecheza michezo saba, Phelan, atakua uwanjani kesho na kikosi chake kusaka alama tatu muhimu kwa kucheza na Fc Bournemouth.