Norway yakataa kuizawadi Finland mlima

Kilele cha mlima Halti hupatikana mita 20 kutoka mpakani Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Kilele cha mlima Halti hupatikana mita 20 kutoka mpakani

Norway imekataa pendekezo la kukabidhi kilele cha mlima kwa jirani yake Finland kama zawadi, taifa hilo linaposherehekea miaka 100 tangu kujipatia uhuru wake kutoka kwa Finland.

Kumekuwa na kampeni kwenye mitandao ya kijamii kutaka taifa hilo lisalimishe kilele cha mlima Halti. Kilele cha mlima huo kipo mita 20 ndani ya ardhi ya Norway.

Mpaka wa mataifa hayo mawili hupitia kwenye mlima huo karibu na kilele.

Waziri mkuu wa Norway Erna Solberg amesema katiba ya nchi yake inaharamisha hatua yoyote ya kusalimisha ardhi ya Norway.

Waliokuwa wakiendesha kampeni walikuwa wanasema kuhamisha kilele cha mlima huo ambacho kinapatikana mita 1,330 juu ya usawa wa bahari hakiwezi kusababisha mabadiliko makubwa kwenye ramani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waliotaka Finland ipewe kilele hicho kama zawadi wanasema ingewa "zawadi nzuri sana".

Wanasema haitakuwa hasara kubwa sana kwa Norway kwani taifa hilo tayari lina milima mingi mirefu.

Ukurasa wa Facebook ulioanzishwa kusaidia kampeni hiyo umependwa na watu 17,000 kufikia sasa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii