Nyumba ya Adolf Hitler kuvunjwa Austria

Nyumba ya Hitler nchini Austria
Image caption Nyumba ya Hitler nchini Austria

Nyumba nchini Austria ambayo Adolf Hitler alizaliwa inatarajiwa kuvunjwa ili kuzuia kuwa kituo cha wanachama wa Nazi.

Hatma ya nyumba hiyo ilijadiliwa huku kukiwa na mgawanyiko wa maoni wa kuivunja ama kubadilisha matumizi yake.

Mjadala huo ulitatiza baada ya mmiliki wa jumba hilo kukataa kuiuza.

Lakini waziri wa maswala ya ndani Wolfgang Sobotka alisema kuwa kamati ya wataalam iliamua kwamba nyumba hiyo ivunjwe,kulingana na gazeti moja la Austria.

Jumba jipya litakalojengwa litatumika kwa maswala ya utawala ama hisani gazeti hilo liliongeza.