UNESCO lapitisha azimio la Jerusalem linaloikera Israel

Azimio hilo la nchi za kiarabu linashutumu shughuli za Israel katika ukingo wa magharibi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Azimio hilo la nchi za kiarabu linashutumu shughuli za Israel katika ukingo wa magharibi

Shirika la Umoja wa mataifa la utamaduni UNESCO limeidhinisha azimio linalozusha mzozo ambalo halihusishi uhusiano wa Wayahudi na eneo takatifu Jerusalem.

Bodi kuu ya Unesco imeidhinisha azimio hilo lililofadhiliwa na nchi za kiarabu, ambalo linataja mara kwa mara jina la kiislamu la eneo takatifu ambalo pia ni eneo takatifu kwa wayahudi.

Kwa wayahudi, eneo hilo linajulikana kama Temple Mount na kwa waislamu linajulikana kama Haram al-Sharif.

Azimio hilo limesababisha Israel kusitisha ushirikiano na Unesco wiki iliopita.

Dhamira iliyotajwa ni "kulinda utamaduni wa Palestina na mandhari ya Jerusalem mashariki".

Linashutumu shughuli za Israel katika maenoe takatifu Jerusalem na ukingo wa magharibi uliokaliwa na walowezi wa kiyahudi.

Haki miliki ya picha AFP

'Kucheza Mchezo'

Lakini suala ni namna inavyotaja maeneo hayo takatifu iliosababisha Israel kuchukua hatua dhidi ya shirika hilo la kitamaduni.

Wakati limetambua umuhimu wa mji wa kale wa Jerusalem na kua zake kwa dini tatu", Azimio hilo limetaja eneo ilo takatifu mlimani kwa jina "msikiti al-Aqsa/al-Haram al-Sharif" (eneo tukufu).

Ni eneo la mahekalu mawili ya Wayahudi a limezibwana ukuta wa magharibi, uliojengwa na Wayahudi kama sehemu ya ukuta uliokuwepo wa eneo la hekalu hilo.

Haram al-Sharif ni eneo pia ambako waislamu wanaamini Mtume Muhammad alikwea mbinguni na eneo la tatu takatifu katika dini ya kiislamu.

Azimio hilo linataja eneo la mbele ya ukuta huo kama "ukuta wa al-Buraq" 'ukuta wa magharibi' - kuweka alama ya mabano mara moja kwa 'ukuta wa magharibi' kama inavyofahamika kwa Wayahudi na hivyo kulipa jina hilo uzito mdogo kuliko jina linalotumika na waislamu,"ukuta wa al-Buraq".

Mwenyekiti wa bodi kuu ya Unesco Michael Worbs amesema angependelea muda zaidi kushughulikia makubaliano.