Kimbunga Haima kuleta uharibifu mkubwa Ufilipino

Kimbunga Typhoon Haima katika picha za satelite
Image caption Kimbunga Typhoon Haima katika picha za satelite

Watabiri wa hali ya hewa wamesema kuwa maharibiko makubwa yatatokea Ufilipino kutokana na kimbunga Typhoon Haima, ambacho kitaambatana na upepo mkali pamoja na mvua katika kisiwa cha Luzon kaskazini kwa nchi hiyo.

Kimbunga hicho kimekadiriwa kuwa ni kimbunga cha hali ya juu kabla ya kuwasili kwake.

Rais Rodrigo Duterte, ambaye yupo ziarani nchini Uchina kwa sasa amesema huduma za hali ya hatari tayari zimepangiliwa.

Makumi kati ya maelfu ya raia wapo katika makazi ya muda.