Rais Maduro ashutumiwa kukataa kura ya maoni

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ameapa kutofanyika kura ya maoni mwaka huu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ameapa kutofanyika kura ya maoni mwaka huu

Wabunge wa upinzani nchini Venezuela wametangaza kuwa serikali ya Rais Nicolas Maduro imefanya mapinduzi ya kijeshi kwa kuzuia kura ya maoni ya kumwondoa madarakani.

Katika kikao kilichojawa na kelele na kuingiliwa na wafuasi wa bwana Maduro, wabunge hao wamepiga kura kuwa serikali imevunja katiba. Na kuahidi kuitisha maandamano kwa wananchi ili wapinge maamuzi hayo.

Wiki iliyopita Tume ya Uchaguzi ya Venezuela iliahirisha upigaji wa kura ya maoni kwa madai ya udanganyifu uliofanywa na upinzani. Uungwaji mkono wa bwana Maduro unapungua hasa ikizingatiwa kwamba nchi hiyo inakumbana na janga la ukosefu wa chakula, mfumko wa bei na kuongezeka kwa uhalifu.

Lakini Rais Maduro amegoma kuachia madaraka kwa takribani mwaka mmoja tangu jitihada za kumwondoa madarakani kuanza kufanyika.