Mfalme wa Morocco kukutana na Magufuli

Rais Magufuli na Mfalme Mohamed Haki miliki ya picha Ikulu, Tanzania
Image caption Rais Magufuli akimlaki Mfalme Mohamed VI uwanja wa ndege wa Nyerere, Dar es Salaam

Mfalme wa Morocco Mohammed VI yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ambapo miongoin mwa mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Mfalme Mohammed VI aliwasili Tanzania Jumapili akitokea nchini Rwanda.

Atafanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadaye wawili hao watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Morocco.

Haki miliki ya picha Ikulu, Tanzania
Image caption Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara walioandamana na Mfalme Mohamed VI

Mfalme huyo ameandamana na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara.

Morocco inatafuta pia uungwaji mkono katika juhudi zake za kutaka kurejea katika Umoja wa Afrika (AU).

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii