Kelele zamuondoa Justin Bieber jukwaani kwa hasira

Justin Bieber
Image caption Justin Bieber

Justin Bieber aliondoka katika jukwaa la tamasha yake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati anapoimba.

Wakati wa tamasha zake tatu zilizopita katika mji huo ikiwa miongoni mwa ziara yake ya dunia nzima mwanamuziki huyo alisema : Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi munayonipa na nathamini ukarimu wenu.Lakini kelele munazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe.Tafadhali na ahsanteni.Sidhani ni muhimu ninapojaribu kusema kitu na nyinyi munapiga kelele.

Na mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele zao aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa,huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.

Image caption Justin Bieber

Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha yake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.

''Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho ,munajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.