Bunge la Venezuela kufungua kesi dhidi ya Rais Maduro

Nicolas Maduro
Image caption Rais wa Venezuela Nicolas Maduro

Bunge nchini Venezuela limepiga kura ya kufungua kesi ya kisiasa dhidi ya Rais wa Kisosholisti Nicolas Maduro, jambo lililoongeza zaidi mvutano baina ya serikali na upinzani wanaoongoza vikao vya kitaifa.

Bunge hilo limemtuhumu rais Maduro kwa kuvuruga demokrasia na limemwamuru kutokea mbele ya bunge siku ya jumanne ijayo, jambo ambalo wachambuzi wamesema halitawezekana kwa rais Maduro.

Kwa upande wake Rais Maduro amelishitumu bunge hilo kwa mapinduzi. mahakama kuu ya nchi hiyo imesema uamuzi wa bunge kuwa sio wa halali.

Wiki iliyopita upinzani uling'ang'ania kuitishwa kwa kura ya maoni wakitaka kuondolewa madarakani kwa rais Maduro lakini kulisitishwa na mamlaka ya uchaguzi.