Matumaini Mapya ya uhusiano mzuri wa Cuba na Marekani

cuba Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Obama ndiye Rais wa kwanza kutembelea Cuba tangu mwaka 1928

kwa mara ya kwanza nchi ya Marekani , hawakupiga kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya kumaliza kizuizi cha biashara na Cuba. Washington imekua ikipinga makubaliano kwa miaka 24 sasa lakini utawala wa Obama umetumia mbinu laini baada ya kuvunjika kwa uhisiano wa Diplomasia takribani miongo mitano iliyopita.

Azimio lililowasilishwa na Cuba,lilipitiwa na nchi 191 huku Marekani na Urusi hawakupiga kura ya kukubali au kukataa.

Hata hivyo kizuizi hiko kinaweza kuondolewa na bunge la Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodríguez ameielezea hali hiyo kuwa ni hatua nzuri kwa wakati ujao wa kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Cuba.