UN yatahadharisha kuhusu hali Sudan Kusini
Huwezi kusikiliza tena

UN yatahadharisha kuhusu hali Sudan Kusini

Umoja wa mataifa umeonya kuwa hali mbaya ya kibinadamu nchini Sudan Kusini itaendelea kuzorota zaidi katika miezi michache ijayo, wakati kipindi cha kiangazi kinapoanza. Tayari zaidi ya watu milioni tatu wamepoteza makazi kutokana na vita.

Mkataba wa amani uliotiwa sahihi mwaka uliopita ulivunjika julai mwaka huu baada ya vita kuzuka nje ya afisi ya Rais. Watalaamu wanasema mkataba huo, na serikali ya umoja wa kitaifa inabakia kuwa tumaini pekee kwa taifa hilo changa.

Mwandishi wa BBC Anne Soy amekuwa katika mji wa Bentiu, na ametuma taarifa ifuatayo