Tom Close, Daktari wa aina yake nchini Rwanda

Huwezi kusikiliza tena
Dr Thomas Muyombo anayejulikana pia kama Tom Close

Tom ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu. Alizaliwa 28 October 1986. Alianza kuimba kwenye Kwaya ya kanisa. Mwaka 2005 Muyombo aliunda kundi lake la kwanza akiwa na marafiki zake wanne wakijiita Afro-Saints.

Wimbo wake wa kwanza akiwa msanii wa kujitegemea ulikuwa Mbwira aliourekodi mwezi Novemba mwaka 2007 kisha mwaka 2008 akaachia Albamu iliyoitwa Kuki. Baadaye alirekodi albamu nne kati ya mwaka 2008 na 2013 zikiitwa Sibeza, Ntibanyurwa, Komeza Utsinde na Mbabarira Ugaruke.

Image caption Tom Close

Anautambua muziki wake kuwa wa mahadhi ya "Afrobeat, Dancehall, Pop na RnB ambayo ina mtindo wa kiafrika.

Image caption Tom Close jukwani

Ameshirikiana na wasanii kadhaa akiwamo Radio na Weasel, General Ozzey, Knowles na hata Sean Kingston. Ametumbuiza kote Afrika mashariki n ahata Marekani na miongoni mwa wanaomvutia ni Chris Brown na Usher Raymond.

Tom Close alichaguliwa kuwa mshindi wa tuzo ya kwanza ya mwaka ya Primus Guma Guma Super Star ambayo hutunukiwa mwanamuziki anayependwa zaidi nchini Rwanda.

Image caption Daktari Thomas Muyombo

Pia ameshinda na kuwa msanii bora wa mwaka katika Salax Awards mwaka 2009, 2010 na 2011.

Zaidi ya muziki na udaktari wa kutibu binadamu aliousomea katika Chuo cha taifa cha Rwanda na kuajiriwa na Hospitali ya Jeshi la Polisi iliyoko Kigali, pia ni mwandishi wa vitabu vya Inka Yanjye, Nkunda u Rwanda, na Isuka Yanjye.