Utumiaji wa mpango wa uzazi wapungua

Aina ya mpango wa uzazi
Image caption Tembe za kupanga uzazi

Idadi ya wanawake na wasichana wanaotumia njiya ya kisasa ya mpango wa uzazi hususan nchi masikini imepita milioni 300.Hii ndio mara ya kwanza kufikia kiwango hiki kwa mujibu wa shirika la kimataifa linaloangazia afya ya uzazi{Family Planning 2020}.

Shirika hilo lilizinduliwa baada ya kongamano la mpango wa uzazi kufanyika mjini London miaka minne iliyopita. Katika ripoti yake 'Family Planning' 2020 imenadi kwamba wanawake milioni 30 wameweza kupokea huduma ya mpango wa uzazi kwa mara yao ya kwanza.

Hata hivyo kungali na mapungufu kadhaa. Licha ya ufadhili kuongezwa kusaidia huduma za mpango wa uzazi, hata hivyo hakuna hatua mpya zilizopigwa. Aidha malengo yaliyowekwa hayawezi kuafikiwa kutokana na takwimu za sasa.

Image caption Tembe zinazozuia mimba

Maeneo ambapo mpango wa uzazi wa kisasa umeimarika ni pamoja na Bara Asia na Kusini mwa Afrika ambapo kwa mara ya kwanza asili mia 30 ya wanawake wanatumia dawa za kisasa za kupanga uzazi.

Hali ni ya kuvunja moyo upande wa Afrika magharibi ambapo mpango wa uzazi wa kisasa haukumbatiwi na wengi.Barani Asia wanawake wengi wameanza kupenga kutumia dawa za kisasa za kupanga uzazi.

Kwa jumla wanawake milioni 225 kutoka nchi masikini hawana huduma hii ya mpango wa uzazi.Wanamazingira wamechangia kwenye suala hili na kusema dunia ina wajibu wa kuwapa nguvu wanawake kusimamia afya yao ya uzazi, kama njiya moja ya kupunguza msongamano na kung'ang'ania raslimali chache zilizobakia duniani.