Ban Ki-Moon amfuta kazi kamanda Mkenya aliyeongoza wanajeshi Sudan Kusini

Ban Ki-Moon Haki miliki ya picha AP
Image caption Ban Ki-Moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemfuta kazi kamanda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa wanajeshi wake walishindwa kuwalinda raia.

Habari za kufutwa kwa Luteni jenerali Johnson Mogoa Kimani Ondieki, ambaye ni Mkenya, zilitangazwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric.

Uchunguzi huo uliungwa mkono na madai ya wafanyikazi wa kutoa misaada, waliosema kuwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walikataa kuitikia wito, wakati wanajeshi wa serikali walishambulia makao ya shirika la kimataifa la kutoa misaada wakati wa mapigano mwezi Julai mjini Juba.

Image caption Mapigano yalizuka Juba mwezi Julai

Wakati wa shambulizi hilo mwandishi wa habari raia wa Sudan Kusini aliuawa na wafanyikazi kadha wa kutoa misaada kupigwa na kubakwa.

Ripoti hiyo ilisema kuwa walinda amani ambao walikuwa umbalia wa kilomita chache, walikuwa wa kutoaminiwa na waoga.