Shirika lapendekeza Yahya Jammeh awekewe vikwazo

Yahya Jammeh Haki miliki ya picha AFP
Image caption Yahya Jammeh aliingia madarakani mwaka 1994 kupitia mapinduzi

Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch alimetoa wito kwa jamii ya kimataifa kumshinikiza zaidi Rais wa Gambia Yahya Jammeh.

Shirika hilo linasema kiongozi huyo amekuwa akiwahangaisha wapinzani wake uchaguzi mkuu wa mwezi ujao unapokaribia.

Kwenye ripoti mpya, shirika hilo linasema wanaharakati wawili wamefariki wakiwa kizuizini na wengine kadha wanazuiliwa gerezani, bila huduma za kimatibabu na mawakili.

HRW wametoa wito kwa majirani wa Gambia pamoja na Umoja wa Ulaya na Marekani kuingilia kari.

Shirika hilo linataka kiongozi huyo pamoja na washirika wake wawekeze vikwazo vya kutosafiri na pia mali yao izuiliwe hadi hali iimarike.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji nchini Gambia mapema mwaka huu

Kadhalika, wanataka taifa hilo litimuliwe kutoka kwa jumuiya ya miungano ya kanda.

Rais Jammeh aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya serikali mwaka 1994.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii