Waandishi wa habari 213 waliuawa duniani mwaka 2015

Waandishi wa habari 213 waliuawa kote duniani mwaka uliopita Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandishi wa habari 213 waliuawa kote duniani mwaka uliopita

Takriban waandishi wa habari 213 waliuawa mwaka uliopita, na kuwa mwaka wa pili ambao waandishi wengi zaidi wa habari waliuawa kwa miaka kumi iliyopita kwa mujibu wa ripoti ya shirika la elimu sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa Unesco.

Barani Afrika waandishi wa habari 16 waliuawa ikilinganishwa na waandishi 1i waliouawa mwaka 2014.

Ripoti hiyo inasema kuwa waandishi wengine wa habari waliuawa kwemye mzozo.

Unesco imetoa ripoti hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ili kutoa hamasisho kuhusu hatari inayowakumba waandishi wa habari

Somalia ambalo ni taifa limekumbwa na mzozo kwa zaidi ya miongo miwili, ni moja na maeneo hatari zaidi duniani kuwa waandishi wa habari.

Takriban waandishi wa habari 53 waliuawa nchini humo kati ya mwaka 2006 na 2015 hasa kwa njia ya kulengwa.