Soyinka: nitairarua green card yangu ikiwa Trump atashinda

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Soyinka ni mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986.

Mshindi wa tuzo la Nobel katika fasihi raia wa Nigeria Wole Soyinka, amesema kuwa atairarua green card yake ambayo inamruhu kuishi nchini Marekani ikiwa mgombea wa Republican Donald Trump atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo wiki ijayo.

Akizungumza kwenye chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza, Soyinka alisema kuwa licha ya kutokuwepo uwezekeno wa Trump kushinda lakini kama atashinda, basi kitu cha kwanza atakachokifanya ni kuwataka wale wote walio na green-card kutuma maombi upya ili kuweza kupata kibali cha kuingia tena Marekani.

"Kwa hivyo singojei hilo," Soyinka alinukuliwa akisema.

"Mara watakapomtangaza kuwa mshindi, nitairarua green card yangu na kuanza kufunganya virago," aliongeza Soyinga.

Bwana Soyinka ni msomi katika chuo cha masuala ya Afrika mjini New York.

Alikuwa mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986.