Kiongozi wa IS asema hawatauachilia mji wa Mosul

Abu Bakr al-Baghdadi Haki miliki ya picha 'IS' VIDEO
Image caption Abu Bakr al-Baghdadi

Kundi la Islamic State limetoa kanda ya sauti ambayo linasema kuwa ni kutoka kwa kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi.

Ikiwa ni ukweli utakuwa ni ujumbe wa kwanza kutoka kwake katika kipindi cha mwaka mmoja, na huenda ukamaliza uvumi kuwa aliuawa.

Sauti hiyo inawataka watu nchini Iraq kulinda mji wa Mosul dhidi ya jeshi la Iraq, ambao linajaribu kuukomboa kutoka kwa wanamgambo wa Islamic State.

Mahala alipo Baghdadi hapajulikani. Baadhi ya maafisa wanasema kuwa huenda yuko ndani ya mji wa Mosul pamoj na wapiganaji wa Islamic State.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi la Iraq linashirikiana na vikosi vingine kuteka mji wa Mosul

Haijabainika ikiwa saudi hiyo ni ya Baghdadi. Kuna uvumi kuhusu kuuawa kwake miaka iliyopita, ikiwemo mwaka uliopita wakati jeshi la Iraq lilisema kuwakuwa lilishambulia msafara wake.

Mosul ambayo ni ngome ya mwisho ya Islamic State nchini Iraq ndio mji Baghadadi alitangazia kujitawala miaka miwili iliyopita.

Mosul, the last IS urban stronghold in Iraq, is where Baghdadi declared a caliphate two years ago.

Abu Bakr al-Baghdadi au nee Ibrahim Awwad Ibrahim al-Badri, alizaliwa mwaka 1971 kwenye familia ya kusinni eneo la Samara nchini Iraq.