Kipa wa timu ya soka ya taifa nchini Gambia afa maji

Hadi kifo chake, Fatim Jawara, alikuwa na umri wa miaka 19 Haki miliki ya picha GFF
Image caption Hadi kifo chake, Fatim Jawara, alikuwa na umri wa miaka 19

Shirikisho la kandanda nchini Gambia, linasema kwamba kipa wa timu ya taifa ya soka ya wanawake, amekufa maji baada ya kuzama alipokua akijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean, katika harakati za kutafuta maisha mazuri barani Ulaya.

Inasemekana aliondoka Gambia miezi miwili iliyopita na kuvuka jangwa la sahara hadi Libya, ili kuabiri boti na kuvuka bahari hiyo.

Alijaribu kuingia bara Ulaya kwa kutumia boti, lakini boti hilo likakumbwa na hitilafu baharini na kuzama.

Hadi kifo chake, Fatim Jawara, alikuwa na umri wa miaka 19.

Taifa dogo la Gambia, ambalo lina idadi ya watu milioni mbili, ni mojawepo ya mataifa ambayo wahamiaji wengi wanatoroka na kuingia nchini Italia.

Watu wengi wanatoroka ugumu wa maisha, na kunyanyaswa na serikali.

Shirika la kimataifa linalowashughulikia wakimbizi- IOM, linasema kuwa mwaka huu pekee, wahamiaji wapatao elfu nne wamefariki dunia, wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean.