Mlipuaji ashambulia msafara wa magari Somalia

Mlipuaji ameshambulia msafara wa magari Somalia na kuwaua watu wawili
Image caption Mlipuaji ameshambulia msafara wa magari Somalia na kuwaua watu wawili

Watu wawili wameuawa baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga kushambulia msafara wa majeshi karibu na bunge la Somalia mjini Mogadishu.

Vyombo ya habari nchini humo vimeripoti kuwa idadi ya waliyouawa katika shambulio hilo huenda ikawa juu zaidi.

Kundi la kigaidi la al-Shabab limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Kundi hilo ambalo wakati mmoja lilikuwa limeteka maeneo mengi ya Somalia linataka kuiong'oa madarakani serikali ya sasa mjini Mogadishu, inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa kwa lengo la kuwafurusha walinda amani wa Umoja wa Afrika.

Burundi imetishia kuwaondoa wanajeshi wake katika kikosi cha kulinda amani cha umoja huo nchini Somalia.