Utabiri wa TB Joshua waambulia patupu

TB Joshua ni muhubiri maarufu zaidi na tajiri nchini Nigeria Haki miliki ya picha AFP
Image caption TB Joshua ni muhubiri maarufu zaidi na tajiri nchini Nigeria

Utabiri wa mhubiri maarufu raia wa Nigeria TB Joshua, kuwa Hillary Clinton atamshinda Donald Trump umeambulia patupu

Aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa Bi Clinton atashinda kwa kura chache. Kwa sasa ujumbe aliouandika kwenye mtandao umefutwa na sasa watu wanaendelea kumkejeli mhubiri huyo.

TB Joshua ni mmoja wa wahubiri maarufu na wenye kukumbwa na utata barani Afrika huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa utabiri wake ni wa ukweli.

Image caption Watu kutoka kote duniani hufika kanisa lake kupata uponyaji

Sawa na wahubiri wengine nchini Nigeria, TB Joshua ni tajiri na mwenye ushawishi mkubwa.

Watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia husafire hadi kanisa lake nchni Nigeria kutibiwa na kushuhudia unabi wake.

Wakati ugonjwa wa Ebola ulikumba eneo la magharibi mwa Afrika, mamlaka ya mji wa Lagos ilitangaza kuwa hakuna mgonjwa wa ugonjwa wa ebola angepelekwa kanisani humo kuponywa. Hii ilikuwa ni hatua ya kuzuia maambukizi

Image caption TB Joshiua ni mmoja wa wahubiri matajiri zaidi nchini Nigeria

Baada ya kifo cha Michael Jackson, mhubiri huyo alidai kuwa hilo ni suala ambalo alikuwa amelizungumzia miezi sita kabla.

Wakosoaji wake wameutaja utabiri wake kuwa uongo. Hata hivyo hilo halijawazuia wafuasi wake kufurika kanisani mwake kutafuta mwelekeo.