Mwanamke wa Afghanistan mwenye macho ya kushangaza atimuliwa Pakistan

Sharbat Gula asindikizwa na polisi kuondoka hospitalini kabla ya kusafirishwa hadi mpakani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sharbat Gula asindikizwa na polisi kuondoka hospitalini kabla ya kusafirishwa hadi mpakani

Mwanamke kutoka Afghanistan aliyepata umaarufu duniani picha yake ilipochapishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa jarida la National Geographic mwaka 1985 alipokuwa msichana ametimuliwa kutoka Pakistan.

Hii ni baada yake kupatikana na stakabadhi bandia za utambulisho.

Sharbat Gula amefurusgwa kutoka Pakistan baada yake kutumilia kifungo cha siku 15 jela akiwa hospitalini ambapo amekuwa akitibiwa ugonjwa wa hepatitis C.

Yeye na wanawe wanne wamekabidhiwa kwa maafisa wa Afghanistan mpakani.

Anatarajiwa kukutana na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani mjini Kabul.

Sharbat Gula alitoroka Afghanistan ilipokuwa chini ya utawala wa muungano wa Usovieti.

Picha yake kama mkimbizi, ambapo alionekana kuwa na macho makali, iliibuka kuwa kama nembo ya madhara ya vita Afghanistan.

Macho yake yalikuwa na rangi ya kijani, jambo lililomfanya kufahamika kwa jina 'Green-eyed Girl'.

Haki miliki ya picha Steve McCurry / Magnum Photos
Image caption Sharbat Gula alikuwa na miaka 12 alipopigwa picha iliyopata umaarufu

Baada ya kukamatwa kwake eneo la Peshawar, karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan tarehe 23 Oktoba, alikiri makosa yote na akapigwa faini ya rupia 110,000 ($1,100).

Alikabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela miaka kadha.

Pakistan ilianza kuwasaka watu wenye vitambulisho bandia majuzi huku uhusiano wake na Afghanistan na India ukidorora.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sharbat Gula, aonekana awali kabla yake kutimuliwa kutoka Pakistan

Picha maarufu ya Bi Gula ilipigwa 1984 alipokuwa kambi ya wakimbizi kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Wakati huo wanajeshi wa Muungano wa Usovieti walikuwa wameingia Afghanistan.

Mwaka 2002, mpiga picha Steve McCurry alimtafuta na kumpiga picha. Wakati huo alikuwa anaishi kijiji kimoja Afghanistan akiwa na mumewe na binti zao watatu.

Baada ya kutokea kwa habari za kukamatwa kwa Bi Gula, Bw McCurry alisema atafanya kila juhudi kumsaidia kifedha na kisheria.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Sharbat Gula alipigwa picha na Steve McCurry (pichani), ambaye miaka 17 baadaye alimtafuta na kumpiga picha nyingine

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii