California yahalalisha utumizi wa bangi kujiburudisha

Jimbo la California limehalalisha utumizi wa bangi kujiburudisha
Image caption Jimbo la California limehalalisha utumizi wa bangi kujiburudisha

Wapiga kura katika jimbo la California,Nevada na Massachusetts wameidhinisha sheria ya kujiburudisha kwa kutumia bangi katika uchaguzi uliokwenda sambamba na uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Kura hiyo inahalalisha ukuzaji wa bangi na utumizi wake kwa wale walio juu ya umri wa miaka 21.

Matokeo katika jimbo la Maine hayajulikani ,huku Arizona ikikataa kuhalalisha utumizi wa bangi kujiburudisha.

Raia wa Florida na Dakorta Kaskazini walipitisha utumizi wa bangi kama dawa.

Dawa hiyo itatumika katika kukabiliana na magonjwa kama vile saratani ,ukimwi na Hepatatis C.

Jimbo la California limesema kuwa kodi inayotozwa katika uuzaji na ukuzaji wa bangi itatumika kusaidia miradi ya vijana ,uhifadhi wa mazingira pamoja uimarishaji wa sheria.