Yanga yaichapa Ruvu Shooting

Yanga Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara wana wajangwani Yanga, wamemaliza michezo ya mzunguko kwanza kwa ushindi dhidi ya Ruvu Shooting.

Yanga walipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa katika dimba la uhuru Jijini Dar es Salaam.

Ruvu Shooting ndio walianza kuzifumani nyavu za Yanga kwa bao la Abdulrahman Mussa kwenye dakika ya saba ya mchezo.

Winga wa Yanga Simon Msuva akaisawazishia timu yake bao hilo kwenye dakika ya 32, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga goli la pili na la ushindi katika dakika ya 56 kipindi cha pili.

Yanga wanasalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 33, huku wapinzani wao Simba wakiwa kileleni kwa alama 35.

Ligi kuu inasimama kwa muda na mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Desemba, mwaka huu.