Picha tano za kusisimua mkutano wa Trump na Obama

Rais mteule wa Marekani Donald Trump alipokutana na Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza ikulu ya White House tangu ashinde uchaguzi, uadui kati yao ulijidhihirisha.

Bw Trump kwenye kampeni alimweleza Bw Obama kama rais mbaya zaidi kuwahi kuongoza Marekani.

Rais Obama naye alisema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.

Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na alikejeliwa hadharani na Rais Obama.

Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu kuficha uadui kati yao.

Waliongea maneno mazuri kuhusu umoja na umuhimu wa kupokezana madaraka kwa amani.

Lakini picha zilizopigwa zinaonesha jambo tofauti, ukiangalia sura na mikono...

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nikiangalia sana pale mbali, haya masaibu yote yatapita...
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Fikira za Trump zinaonekana kuyumba ... labda kwa kukumbuka aibu iliyotokana na utani kuhusu kuzaliwa kwa Obama mwaka 2011.
Haki miliki ya picha European photopress agency
Image caption Wanasalimiana lakini macho yako wapi.... taama mdomo wa Trump
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tena, sasa Obama anamwangalia Trump.... lakini Trump anaamua, la hasha, SIWEZI kumwangalia machoni
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kupeana mikono kwisha sasa, na ni furaha sana kwa Trump .... lakini anaonekana kutoyaamini anayoyasema Rais Obama

Lakini yote hayakuwa kununa tu...

Haki miliki ya picha European photopress agency
Image caption Wawili hao walicheka wakati mmoja walipotaniana.

Melania na Michelle pia walikutana, lakini hawakuonekana kuwa na matatizo

Haki miliki ya picha White House
Image caption Melania Trump na Michelle Obama wakiwa ikulu ya White House

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii