Mambo matano ya kipekee uchaguzini Marekani

Dixville Notch Haki miliki ya picha EPA

Wamarekani walimchagua mwanachama wa Republican Donald Trump kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo, ambapo alimshinda mgombea wa Democratic Hillary Clinton kwenye uchaguzi uliofanyika Novemba 8.

Wapiga kura katika majimbo 50, pamoja na eneo la Washington DC, walipiga kura katika nyakati sita tofauti, kutokana na ukubwa wa taifa hilo.

Haya hapa ni mambo matano ya kipekee kuhusu uchaguzi Marekani.

Kijiji kidogo New Hampshire hupiga kura kwanza

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images

Tangu 1960, wapiga kura katika kijiji cha Dixville Notch wamekuwa wakipiga kura za kwanza Marekani siku ya uchaguzi, kila inapotimia saa sita usiku.

Mwaka huu, wanaume watano na wanawake wawili walipiga kura. Mtu wa nane alipiga kura kupitia posta.

Hillary Clinton alimshinda Donald Trump, akipata kura nne na Trump mbili. Kura hiyo nyingine ilimwendea Gary Johnson.

Vijiji vingine viwili New Hampshire pia vilipiga kura saa sita usiku.

Mmarekani alipiga kura kutoka anga za juu

Haki miliki ya picha EPA

Mwana anga za juu wa Nasa Shane Kimbrough, ambaye yupo katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu, alipiga kura yake kutoka anga za juu kupitia kituo kilichopo Houston, Texas.

Mwenzake Kate Rubins pia alipiga kura kutoka anga za juu wiki chache zilizopita, kabla yake kurejea duniani Jumapili.

Sheria ilipitishwa Texas mwaka 1997 kuwezesha watu kupiga kura wakiwa nje ya dunia.

David Wolf alikuwa Mmarekani wa kwanza kupiga kura kutoka anga za juu mwaka huo.

Wabunge wanaweza kumchagua rais

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majengo ya Bunge la Wawakilishi mjini Washington DC

Ikitokea kwamba kuwe na mgombea urais ambaye hajapata wingi wa kura za wajumbe (270), basi wabunge wa Bunge la Wawakilishi ndio huamua.

Kwa sasa bunge hilo lina wabunge 435. Chama chenye wabunge wengi bila shaka kitamchagua mgombea wake.

Haki miliki ya picha Netflix

Iwapo wewe hufuatilia House of Cards, Frank Underwood anayeigizwa na Kevin Spacey ni mmoja wa wajumbe wa jimbo la Carolina Kusini.

Makamu wa rais huchaguliwa na Seneti.

Hili limewahi kutokea wakati mmoja pekee, mwaka 1804, wagombea wanne walipogawana sana kura.

John Adams, aliyekuwa wa pili, alichaguliwa rais na Bunge badala ya Andrew Jackson aliyekuwa anaongoza kwa wingi wa kura.

Uchaguzi hufanyika Jumanne Novemba

Tangu 1845, uchaguzi mkuu Marekani umekuwa ukifanyika Jumanne baada ya Jumatatu ya kwanza ya Novemba.

Wengi husema iliamuliwa hivyo kwa sababu ilikuwa wakati wa mavun majira ya kupukutika kwa majani na si karibu sana na majira ya baridi ambapo inaweza kwua vigumu kwa watu kusafiri kutokana na hali ya hewa.

Haki miliki ya picha Getty Images

Jumanne zamani ilikuwa siku ya kabla ya siku ya soko, maana kwamba wakulima wangesafiri siku moja na kupiga kura kisha kurejea nyumbani na kuuza bidhaa sokoni.

Lakini stakabadhi zinaonesha sababu tofauti, ambapo ilikuwa kupunguza kipindi ambacho uchaguzi unaweza kufanyika, kutoka siku 34 hadi siku sita.

Kwa sababu ya sheria hiyo, uchaguzi lazima ufanyike kati ya 2 na 8 Novemba katika miaka inayoweza kugawika na nne bila masalio.

Kuna Wamarekani wengi wasiopiga kura

Marekani inamiliki maene mengi kama vile - Puerto Rico, Guam, Northern Mariana Islands, na Visiwa vya Virgin vya Marekani na Samoa ya Marekani. Wakazi wa maeneo hayo huwa hawapigi kura.

Haki miliki ya picha Getty Images

Aidha, wafungwa, ila katika majimbo ya Maine na Vermont, huwa hawapigi kura sawa na watu wasio na vitambulisho.

Mashahidi wa Yehova, waumini wa dini ya Jehovah Witnesses, pia huwa hwawapigi kura za urais kwa sababu za kidini.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii