Bomu lalipuka nje ya kambi ya jeshi Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la Nigeria lilihamisha makao yake kwenda mji wa Maiduguri

Bomu limelipuka nje ya kambi ya jeshi iliyo mmji ulio Kaskazini Mashariki mwa Nigeria Maiduguri.

Walioshuhudia wanasema kuwa karibu milipuko mitatu au minne mikubwa ilisikika karibu na kambi ya Maimalari leo asubuhi.

Rais Muhammadu Buhari alihamisja makao makuu ya kijeshi kwenda mji wa Maiduguri mwaka uliopita ili kuweza kukabiliana vilivyo na kundi la Boko Haram.

Wanamgambo hao wa kiislamu wamepoteza ardhi kubwa ambayo walikuwa wameidhibiti katika kipindi cha miezi 20, lakini wamehusika kwenye mashambulizi kadha pamoja na ya kujitoa mhanga