Kifaa kutoka angani chaanguka Myanmar

Kifaa hicho kina urefu wa mita 4.5 na upana wa mita 1.2. Haki miliki ya picha Yannaing Pyi Sone Aung
Image caption Kifaa hicho kina urefu wa mita 4.5 na upana wa mita 1.2.

Kifaa kikubwa cha chuma kimeanguka kutoka angani katika eneo la migodi Kaskazini mwa Myanmar

Kifaa hicho cha muundo wa mviringo, kilichopatikana siku ya Ijumaa katika jimbo la Kachin, kina urefu wa mita 4.5 na upana wa mita 1.2.

kifaa kingine cha chuma chenye maandishi ya kichina kilitoboa paa la nyumba iliyo karibu wakati mmoja lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Inakisiwa kuwa kisa hicho huenda kinahusiana na satellite ya China iliyorushwa angani.

Wakaazi walisema kuwa walisikia sauti kubwa kabla ya kifaa hicho kuanguka

Maafisa kutoka kwa idara moja ya ulinzi iliyo karibu, wanasema kuwa kifaa hicho kilipingirika umbali wa mita 50 kabla ya kutua eneo moja lenye matope .

"Tulishikwa na hofu kwa sababu ya mlipuko huo," mwanakijiji Ko Maung aliliambia gazeti la Myanmar Times.

Vifa hivyo vinaaminiwa kuwa vya satellite au sehemu za injini ya nge au kombora.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii