Wafungwa miaka 10 kwa kufuja pesa za uzeeni Uganda

Maafisa 3 wahukumiwa miaka 10 jela kwa kufuja pesa za hazina ya uzeeni Uganda
Image caption Maafisa 3 wahukumiwa miaka 10 jela kwa kufuja pesa za hazina ya uzeeni Uganda

Maafisa watatu wa vyeo vya juu nchini Uganda wame hukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa ufujaji wa karibu Dola milioni ishirini na tano,kutoka hazina ya malipo ya uzeeni.

Mahakama moja mjini Kampala imewapata maafisa hao na makosa ya kuelekeza malipo ya uzeeni ya zaidi ya watu elfu mbili, katika akaunti zao za kibinafsi.

Mahakama hiyo aidha imesema watatu hao wanaweza kukata rufaa dhidi ya huku hiyo. Maafisa wengine watano wa vyeo vya chini katika hazina hiyo ya uzeeni, pia wanatarajiwa kushtakiwa wa makosa sawia na hayo.