Le Pen: Ushindi wa Trump ni matumaini kwangu

Marine Le Pen ameiambia BBC kwamba ushindi wa Donald Trump nchini Marekani umemuongezea fursa ya kuchaguliwa kuwa rais Ufaransa
Image caption Marine Le Pen ameiambia BBC kwamba ushindi wa Donald Trump nchini Marekani umemuongezea fursa ya kuchaguliwa kuwa rais Ufaransa

Kiongozi wa mrengo wa kulia nchini Ufaransa Marine Le Pen ameiambia BBC kwamba ushindi wa Donald Trump nchini Marekani umemuongezea fursa ya kuchaguliwa kuwa rais wa Ufaransa mwaka ujao.

Bi Le Pen amesema wimbi la vugu vugu la uzalendo linazidi kushika kasi dhidi ya uongozi uliyopo na kwamba ana imani atashinda uchaguzi ujao.

Akitaja mfano wa Uingereza kujiondoa kutoka muungano wa Ulaya na utawala wa Trump huko Marekani amesema Wafaransa nao watafuata mkondo huo.

Le Pen aidha amesema chini ya uongozi wake hatawapokea wahamiaji zaidi.