India yaongeza kiwango cha utoaji wa fedha

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia wa India wakisubiri kutoa pesa

Serikali ya India imeongeza kiwango cha utoaji wa fedha kufuatia dhadabu kubwa ya umma kwa kuondolewa kwa noti za rupee 500 na 1000 nchini India wiki iliyopita.

Wateja wanaweza kutoa hadi rupee 2,500 kwa siku katika mashine za kutoa pesa za ATM badala 2,000 waziri wa fedha amesema.

Mashine nyingi za kutoa pesa, hazifanyi kazi , kutokana na noti mpya za rupee 500 na 2,000 kuanzishwa.

Milolongo mirefu imeshuhudiwa katika benki nyingi na kusababisha ugumu wa utoaji wa pesa.

Serikali imesema benki za India zimepata rupee trilioni 3(($44bn, £35bn) kwa viwango vikubwa vya noti tangu uhamisho huo kutangazwa siku ya Jumanne usiku.

Upigaji marufuku wa noti za rupee 500 na 1,000 ni njia ya kukabiliana na ulaji wa rushwa na kurudisha mabilioni ya madola ya utajiri ambayo hayajahesabiwa kwa uchumi wa taifa hilo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rupee

Benki kuu ya India imewahimiza raia nchini humo kutoficha pesa , akiongeza kwamba rupee bado ziko 'wakati wowote wanapohitaji'.

Benki hiyo, imezisihi benki kuripoti kila siku kiwango cha fedha kilichotolewa na kubadilishwa ili kupata picha kamili ya jinsi pesa hizo zinavyozunguka.

Waziri mkuu Narendra Modi amekiri 'uchungu' ambao mamilioni ya watu wanapitia lakini amesema 'mpango huo haukuanzishwa bila msingi wowote'.