Nigeria kuuza viwanda vya mafuta

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viwanda vya mafuta vya Nigeria kwa kiwango kikubwa vimekuwa visivyo na faida

Serikali ya Nigeria ina mipango ya kuuza viwanda vya mafuta visivyo na faida.

Taarifa iliyotolewa na serikali ilisema kuwa viwanda hivyo vya kusafisha mafuta vitapewa muda wa kuimarika kabla la kuuzwa.

Nigeria ina viwanda vinne tu vya kusafisha mafuta, na hununua asilimia kubwa ya bidhaa za mafuta licha ya kuzalisha karibu mapipa milioni mbili ya mafuta kwa siku.

Viwanda vya mafuta vya nchi hiyo kwa kiwango kikubwa vimekuwa visivyo na faida.

Kuuzwa kwa viwanda hivyo ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuifanyia mabadiliko sekta ya mafuta nchini humo

Pia serikali ya Nigeria ina mpango ya kubuni msimamizi mmoja wa sekta ya mafuta ambayo itakuwa ni tume ya mafuta.