Malkia wa Ashanti afariki dunia

Malkia wa jamii ya Ashanti Haki miliki ya picha Graphic Online
Image caption Nana Afia Kobi Serwaa Ampem

Malkia wa Ufalme wa jamii ya Ashanti nchini Ghana amefariki dunia akiwa na miaka 109. Nana Afia Kobi Serwaa Ampem wa pili ameongoza ufalme wa jamii hiyo kwa miaka 39.

Wadhifa huu huwa na ushawishi mkubwa katika mila na desturi za jamii hii. Malkia huyu alikua mama wa jamii nzima ya Ashanti na alisimamia masuala yote ya wanawake. Huchaguliwa na wazee wa ukoo wa Oyoko mmoja wa koo nane zinazounda jamii ya Ashanti.

Mfalme au Malkia huongoza hadi kifo.

Pia Malkia huyu alikua na jukumu la kumteua mrithi wake wakati akiondoka. Mwaka wa 1999, alimteua mwanawe wa kiume, Otumfuo Osei wa pili kuwa mfalme wa sasa wa jamii ya Ashanti.

Malkikia Nana Afia Kobi wa 13 alifariki dunia wakati akiwa amelala.Machifu wa ufalme huo watakutana Alhamisi ya wiki hii kuanza mipango ya mazishi yake.