Ushindi wa Trump wamlazimu kubadili jina

Mwanamuziki Nico Segal anayejiita Donnie Trumpet
Image caption Mwanamuziki Nico Segal anayejiita Donnie Trumpet

Mwanamuziki mmoja amebadilisha jina lake la muziki kufuatia ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani.

Donnie Trumpet ,ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kundi la SaveMoney akishirikiana na Chance na Vic Mensa sasa anataka kuitwa kwa jina lake Nico Segal badala yake.

Mwanamuziki huyo amabaye aliwahi kuteuliwa kuwania tuzo ya Grammy aliandika kwamba hakutaka kutoeleweka .

Hii ni baada ya jina analotumia kuhusishwa na lile la rais mteule Marekani Donalds Trump.

Image caption Mwanamuziki Nico akipuliza tarumbeta

Katika chapisho lake la ''kwaheri Donnie'',alielezea kwamba wakati walipokuwa katika ziara ya muziki pamoja na Chance The Rapper ikiwa imesalia siku chache tu kufanyika kwa uchaguzi mkuu alihisi uzito mwilini mwake kutokana na uhusiano ambao watu wanahusisha jina lake na lile la Trump.

Kile kilichoanza kama mzaa kilibadilika na kuwa jambo ambalo sio la mzaha tena

''Ninachoamini sio kile Trump anachoamini....Kutoka sasa niiteni Nico''.