Shinzo Abe akutana na Donald Trump

Japan
Image caption Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amekutana na rais mteule wa Marekani Donald Trump mjini New York na anakuwa kiongozi wa kwanza duniani kukutana na rais huyo.

Rais Trump bado hajaweka bayana mipango na mtazamo wake kwa nchi ya Japan na nchi nyingine za Asia na ahadi zake za uchaguzi kuwafanya washirika wa Marekani kulipa kwenye misaada ya kijeshi.

Upinzani wake wa dhahiri dhidi ya Rais anayeondoka madarakani Barack Obama kuhusiana na masuala ya kibiashara na nchi za Pasific , msingi wa sera za Rais Obama, pia kumeibua maswali yasiyokuwa na majibu hasa barani Asia.

Msemaji wa rais mteule Trump amesema kwamba mkutano baina ya viongozi hao wawili ndiyo mwanzo wa utamaduni usiyo rasmi, kwa sababu Obama angalipo madarakani . Inatarajiwa ziara nyingine baina ya Abe a na makamu wa rais mteule, Mike Pence.