Kwa Picha: Uhusiano wa Obama na Merkel

Merkel na Obama Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Merkel na Obama

Rais wa Marekani Barack Obama yumo katika ziara yake ya sita na ya mwisho nchini Ujerumani akiwa kama rais ambapo amemtaja Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kama rafiki yake wa karibu zaidi kimataifa kwa miaka minane ambayo amekuwa rais.

Uhusiano wao uliwavutia wengi mwaka 2015 kutokana na picha yao (iliyo hapa juu) - iliyotajwa kama iliyodhihirisha "mvuto" kati ya viongozi hao wawili.

Lakini Bi Merkel hakumruhusu Obama kuzungumza katika lango kuu la Brandenburg huko Berlin alipozuru Ujerumani, alipokuwa hajachaguliwa rais mwaka 2008.

Bw Obama alilazimika kutosheka na kukaribishwa katika eneo la Tiergarten.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mjini Berlin

Uhusiano wake kwa siku za kwanza kama rais, ulikumbwa na maoni tofauti haswa kuhusu migogoro ya kifedha duniani, suala kuu lililojadiliwa kwenye mkutano wa G20 ulioandaliwa mjini London.

Barua pepe iliyotumwa kwa Bi Hillary Clinton kutoka kwa washauri wake, iliyoandikwa miezi mitano baadaye, ilisema Bi Merkel hakufurahishwa na ''mazingira yanayomzunguka Obama.''

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama na Merkel

Lakini uhusiano mwema ukaanza.

Wachambuzi kadhaa walisema wawili hao- wakili na mwanasayansi - walipata mbinu bora za uchambuzi na mbinu mbadala za kuangazia sera tofauti.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama na Kansela Merkel

Uhusiano huo ulipata changamoto mwezi Aprili mwaka 2011 pale Ujerumani walipoupinga mpango wa nchi wanachama wa Nato kuishambulia Libya. Lakini mwezi Juni Mwaka 2011, Bi Merkel alitembelea ikulu ya White House na Bw Obama akamkabidhi medali ya Marekani ya Uhuru, na kuongeza kusema Bi Merkel ''ni rafiki yangu wa karibu na mmoja wa mshirika wangu wa karibu zaidi kimataifa''.

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vilichambua usemi huo huku mhariri mmoja akimdadisi kwa kina Bw Obama ''kwa ukarimu wake mkubwa''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama akimkabidhi Merkel medali ya Marekani ya Uhuru,

Kansela Merkel amesema Bw Obama, ni mtu ''mcheshi'' kufanya naye kazi.

Alimkaribisha Obama katika hafla yake ya kwanza mjini Berlin kama rais mwaka 2013.

Wakati huo aliweza kuhutubia umma katika lango kuu la Brandenburg.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama na Merkel

Uhusiano wao ulijaribiwa tena mwezi Oktoba mwaka 2013, wakati nyaraka zilifichuliwa zilizosema kwamba Marekani inawachunguza viongozi wa nchi za kigeni, simu ya kibinafsi ya Kansela wa Ujerumani ikijumuishwa.

Wakati wa ziara ya Merkel kwenye Ikulu ya White House, vyombo vya habari vya Marekani vilisema mkutano na wanahabari huo ulikuwa ''mwenye kibaridi''.

Bi Merkel alikumbana na shida na vyombo vya utafsiri alipotembelea Ikulu hiyo.

Bw Obama alisema alipatwa na ''uchungu'' uliosababishwa na mvutano katika uhusiano wao, uliosababishwa na madai ya uchunguzi wa simu ya Bi Merkel.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bw Obama na Bi Merkel wakihutubia wanahabari

Hivi majuzi, uhusiano kati ya marekani na Ujeremani umeimarika. Wawili hao wamefanya kazi kwa pamoja katika nyanja nyingi ikiwemo, makubaliano ya biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, Ukraine na tatizo la wahamiaji - mambo ambayo Obama amempongeza Bi Merkel kwa kuwa katika "upande sahihi katika historia."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bw Obama na Kansela Merkel

''Kwangu, siku za usoni na rais Obama zina umuhimu sana kuliko siku za hapo awali," Bi Merkel alitangaza hayo mwezi Aprili mwaka 2016, kulingana na shirika la habari la CNN.

Bw Obama amesema : "Huu ni uhusiano muhimu ambao nimekuwa nao katika kipindi changu kama rais."

Kansela Merkel amekuwa na msimamo. Amekuwa imara. Anaaminika. Pia ni mcheshi lakini kwa mara nyingi katika mikutano na wanahabari hadhihirishi hayo yote.''

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama na Markel wakisemezana

Mada zinazohusiana