Mwanamke anayejiita 'mungu' aliyewapiga watu risasi India

Sadhvi Deva Thakur mara nyingi huonekana ameshika bunduki Haki miliki ya picha Manoj dhaka
Image caption Sadhvi Deva Thakur mara nyingi huonekana ameshika bunduki

Polisi nchini India wanamtafuta Sadhvi Deva Thakur, mwanamke aliye mafichoni baabda ya kufyatua risasi za kusherehekea kwenye harusi

Shaghaziye bwana harusi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.

Kwenye video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katia jimbo la Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur anaonekana akifyatua risasi akitumia bunduki aina ya revolver.

Haki miliki ya picha Manoj dhaka
Image caption Hakuna mengi kumhusu Sadhvi

Baadhi ya walinzi wake nao wanaonekana wakifyatua risasi.

Vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa Sadhvi, ambalo ni jina la kiindi linalomaanisha mwanamke aliye mtakatifu au anajiita kuwa mungu alingia sakafuni, ambapo alimuomba DJ kucheza wimbo aliotaka na akaanza kucheza densi.

Wakati huo ufyatuaji risasi ulikuwa ukiendelea.

Haki miliki ya picha Manoj dhaka
Image caption Sadhvi ana wafuasi wachache ambao wengi wengi ni kutoka kijijini

Ripoti zinasema kuwa familia za bibi na bwana harusi zilimuomba awache maombi yao yaliambulia patupu.

Ni wakati shangaziye bwana Harusi mwenye umri wa miaka 50 aliangauka baada ya kupigwa rasasi na wengine watatu kujeruhiwa vibaya, ndipo ufyatuaji huo ukasitishwa.

Wakati huo Sadhvi na walinz wake sita walitoweka. Polisi wamewafungulia kesi ya mauaji na wanajaribu kuwatafuta watu hao saba.