Mashindano ya Tour of Rwanda kuelekea kigali kesho

Image caption Mashindano ya baiskeli ya Tour of Rwanda

Mwendesha baiskeli Eyob Metkel kutoka Eritrea, ndiye aliyeshinda awamu ya tano ya mashindano ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda leo.

Mzunguko huu ulikuwa wa kilomita 125 kutoka mjini Muhanga hadi mji wa Musanze ambako ametumia muda wa saa tatu, dakika 15 na sekunde 57.

Image caption Mashindano ya baiskeli ya Tour of Rwanda

Eyob Metkel anaichezea timu ya Dimension Data ya afrika kusini pamoja na Mnyarwanda Valens Ndayisenga ambaye anaendelea kuongoza mashindano hayo.

Hata hivyo Metkel amefanikiwa kupunguza mwanya uliopo baina yao na sasa Ndayisenga anamzidi tu na sekunde 42.

Image caption Mashindano ya baiskeli ya Tour of Rwanda

Upinzani mkali sasa umeanza kujitokeza ndani ya timu ya Dimension Data ikionekana wazi kuwa mmoja kati ya wachezaji wake huenda akaondoka na ushindi wa Tour of Rwanda.

Kesho mashindano hayo yataendelea, washindani wakitoka mjini Musanze hadi mjini Kigali umbali wa kilomita109.

Image caption Mashindano ya baiskeli ya Tour of Rwanda

Mada zinazohusiana