Wanaume 'wahasiwa' kwa pamoja Nairobi

Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka mjini Nairobi, Kenya.
Image caption Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka mjini Nairobi, Kenya.

Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kupitia upasuaji kwa wanaume (vasectomy), imetangazwa moja kwa moja kutoka chumba cha upasuaji mjini Nairobi, Kenya kama njia ya kuhamasisha watu kuhusu njia hiyo ya kupanga uzazi

Takriban wanaume 150 walifanyiwa upasuaji huo uliodumu muda wa takriban dakika 20 kwa kila mmoja.

Image caption Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka kutoka mjini Nairobi, Kenya.

Madaktari walifanya shughugli hiyo nyuma ya jukwaa lililofunikwa katika ukumbi wa taifa wa sanaa mjini Nairobi.

Wanaume nchini Kenya ambao mara nyingi huwa wana hofu ya kufanyiwa zoezi hilo la kupanga uzazi mara nyingi kwa kuhofia unyanyapaa.

Image caption Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka kutoka mjini Nairobi, Kenya.

Wale wanaoendesha kampeni ya zoezi hilo wanasema kuwa ndiyo njia salama ya kupanga uzazi.

"Wanaume wengi hudhani kuwa zoezi hilo humnadili mwananamme kuwa mwanamke," Jack Zhang ambaye ni daktari kutoka Canada aliiambia BBC.

Baadhi ya wanaume wana hofu kuwa watu hufa kwa wingi barani Afrika kwa hivyo kuna haja ya kuzaa watoto wengi.

Image caption Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka kutoka mjini Nairobi, Kenya.

Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, anasema kuwa baadhi ya wanaume walishiriki zoezi hilo baada ya kuchochewa na gharama ya kulea familia kubwa.

"Mbinu ambazo mke wangu alikuwa akitumia kupanga uzazi, zilikuwa na madhara kwake, kwa hivyo mimi niliamua kwenda kukatwa mirija ya ya uzazi," mwanamme moja aliiambia BBC.