Mhamiaji ajiwasha moto ndani ya benki Australia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mashine ya ATM iliyochomeka ndani ya benki

Mwanamume aliyejiwasha moto ndani ya Benki moja mjini Melbourne, Australia hapo jana ametambuliwa.

Yasemekana mtu huyo anatokea Myanmar na amekuwa akitafuta hifadhi nchini Australia. Habari zaidi zinasema aliwasili nchini humo miaka mitatu iliyopita.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 21 alipelekwa hospitali kupata matibabu chini ya ulinzi wa maafisa wa usalama baada ya tukio hilo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu watano walipata majeraha ya moto na 21 kuathiriwa na moshi

Wanachama wa jamii ya waislamu wa Rohingya mjini Melbourne wamesema mtu huyo aliogopa kurudi Myanmar na kwamba alikuwa anakabiliwa na changamoto za kimaisha.