Makamu wa rais mteule Mike Pence azomewa New York

Huwezi kusikiliza tena
Pence alikuwa amehudhuria tamthilia ya muziki mjini New York

Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alizomewa kwenye ukumbi wa tamthilia mjini New York.

Bwana Pence alikwenda kuona tamthilia yenye muziki, iitwayo Hamilton, inayotokana na maisha ya mmoja kati ya wazee walioanzisha taifa la Marekani, Alexander Hamilton.

Alizomewa kabla na wakati tamthilia inaendelea.

Mwisho wa tamasha, mchezaji mmoja alisoma barua kwa Bwana Pence, kuonesha wasiwasi kuwa serikali mpya hait-linda watu wa rangi, dini na tabia tofauti.