Zaidi ya watu 100 wafariki kwenye ajali ya treni India

Huwezi kusikiliza tena
Waokoaji wanakata mabaki kuwafikia watu waliokwama ndani

Idadi ya watu waliyofariki kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini mwa India, imeongezeka na kupita watu 100 na kuwajeruhi mamia ya wengine.

Treni hiyo ilikuwa ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wengi wa waliokufa walikuwa kwenye mabehewa yaliyokuwa karibu na injini

Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.

Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.