Rais wa Korea Kusini alihusika kwenye ufisadi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano ya kupinga kashfa yamekuwa yakishuhudiwa nchini Korea Kusini

Waendesha mashtaka nchini Korea Kusini, wamegundua kwamba Rais Park Guen Hye, alihusika na kashfa ya ubadhirifu wa pesa za umma inayomkabili rafiki yake wa mda mrefu Choi Sun-Sil.

Wanasema hawana uwezo wa kumfungulia mashtaka rais huyo kwa sababu analindwa na katiba lakini wataendelea kumchunguza.

Bi Choi, anatuhumiwa kwa kutumia usuhuba wake na rais Guen Hye, kuingilia masuala ya uongozi wa taifa hilo, ambapo aliwaamuru wakurugenzi wa mashirika makubwa, kuchangia mamilioni ya pesa wakfu ambao ana uendesha yeye binafsi.

Kashfa hiyo imesababisha maandamano makubwa kwa majuma kadhaa mfululizo.

Mwandishi wa BBC mjini Seoul amesema tangazo hili la sasa, kutoka kwa waendesha mashtaka, huenda likaongeza shinikizo la kumtaka Rais Guen Hye kujiuzulu.