Wahalifu waiangusha ndege ya polisi Brazil

Ghasia zimeendelea kuongezeka mjini Rio katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Haki miliki ya picha AP
Image caption Ghasia zimeendelea kuongezeka mjini Rio katika kipindi cha miaka miwili iliyopita

Maafisa wanne wa polisi wamefariki nchini Brazil baada ya ndege yao aina ya Helikopta kuangushwa na magenge ya wahalifu katika moja ya makaazi makubwa ya mabanda mjini Rio De jenairo.

Ndege hiyo ilikuwa ikisaidia katika oparesheni ya kuwasaka walanguzi wa dawa za kulevya katika mji huo ulioandaa michezo ya olimpiki.

Kumekuwa na ongezeko la ghasia mjini Rio katika kipindi cha miaka miwili iliyopita baada ya mpango uliolenga kuangamiza magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya kufeli.

Ikiwa ndege hiyo ilidunguliwa na magenge ya uhalifu, basi hakitakuwa kisa cha kwanza kweny mji huo ulioandaa mashindano ya olimpiki ya mwaka 2016

Mwaka 2009 walanguzi wa madawa ya kulevya waliifyatulia risasi ndege ya polisi na kusababisha ilipuke kabla ya kuanguka na kuwau marubani wawili.

Ghasia zimeendelea kuongezeka mjini Rio katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kufuatia kufeli kwa programu ya mwaka 2010 ya kupambana na walanguzi wa madawa ya kulevya