Erdogan: Uturuki inaweza kujiunga na Uturuki na China

Haki miliki ya picha ADAM BERRY
Image caption Recep Tayyip Erdogan

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema Uturuki haishughuliki sana kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya, na kukariri kuwa inaweza kuungana na Urusi na Uchina katika jumuia ya Ulaya na Asia.

Vyombo vya habari vya Uturuki vinamnukuu Rais Erdogan akisema, kwamba amelizungumza wazo hilo na mwenzake wa Urusi, Rais Vladimir Putin, na rais wa Kazakhstan, Nursultan Nazarbayev.

Wote ni wanachama katika Mkataba wa Shanghai ,ushirikisho wa kiuchumi na usalama, ambao unajumuisha Uchina, Kyrgyzstan na Tajikistan.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli Uturuki

Matumaini ya Uturuki ya kujiunga Muungano wa Ulaya yalididimia baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli.

Nchi za ulaya zinasema kuwa hatua zilizochukuliwa na Rais Erdogan huenda zikakiuka masharti ambayo Uturuki inastahili kutimiza kuwa mwanachama wa EU.