Watoto kadhaa wauawa shuleni Aleppo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wengi wameuawa Aleppo

Ripoti kutoka eneo la Aleppo linalodhibitiwa na serikali ya Syria, zinaeleza kuwa mizinga iliyorushwa na wapiganaji, imepiga shule, na kuuwa watoto kama saba.

Wanaharakati na vyombo vya habari vya taifa, vinasema mizinga hiyo ilipiga shule katika mtaa wa al-Farqan, magharibi mwa Aleppo, sehemu ya mji inayodhibitiwa na serikali.

Shambulio hilo limefanywa wakati ndege za jeshi zimekuwa zikishambulia kwa mabomu eneo la Mashariki la mji linalodhibitiwa na wapiganaji.

Mashambulio yamekuwa yakiendelea katika siku chache za karibuni, na kuuwa raia zaidi ya mia moja.