Merkel kuwania muhula wa nne

Bi Merkel amekuwa chansela wa Ujerumani tangu mwaka 2005. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bi Merkel amekuwa chansela wa Ujerumani tangu mwaka 2005.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa atawania wadhifa huo tena kwa muhula wa nne.

Merkel mwenye umri wa miaka 62, anatarajiwa kutangaza nia yake hiyo katika makao makuu ya chama cha Christian Democratic Union (CDU).

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika nchini Ujerumani mwaka ujao.

Umaarufu wa Bi Merkel umeshuka tangu lakini bado ana uungwaji mkono mkubwa.

Alipata pigo wakati alishindwa kwenye uchaguzi wa kikanda mapema mwaka huu, na anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama cha mrengo wa kulia cha AfD.

Bi Merkel amekuwa chansela wa Ujerumani tangu mwaka 2005.

Ikiwa atashinda uchaguzi wa mwaka ujao atafikisha rekodi iliyowekwa na Helmut Kohl.