Huenda Romney akateuliwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni

Trump na Romney hawakuzungumza lolote baada ya mkutano wao uliofanyika New Jersey Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump na Romney hawakuzungumza lolote baada ya mkutano wao uliofanyika New Jersey

Makamu wa rais mteule wa Marekani Mike Pence, amethibitisha kuwa Mitt Rombey anaweza kupewa wadhifa wa Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni.

Taarifa hiyo iliyotangazwa na kituo cha Fox News, inajiri baada ya rais Mteule Donald Trump kukutana na bwana Romney, mwanachama wa Republican ambaye alimkosoa wakati wa kampeni.

Kuna uvumi kuwa wadhifa huo ulizungumziwa wakati wa mkutano kati ya viongozi hao.

Hakuna hata mmoja kati yao alitoa taarifa za mkutano wao uliofanyika siku ya Jumamosi.

Mwezi machi wati wa mchujo, bwana Romney alisema kuwa Trump hana tajriba ya kuwa rais naye Trump akajibu kuwa Romney ni mgombea aliyeshindwa.

Huwezi kusikiliza tena
Donald Trump alisema mkutano ulikuwa wenye manufaa.