Upigaji kura wamalizika nchini Haiti

Wahaiti milioni 6.4 wameweza kupiga kura kwa mmoja kati ya wagombea 27
Image caption Wahaiti milioni 6.4 wameweza kupiga kura kwa mmoja kati ya wagombea 27

Upigaji kura unamalizika nchini Haiti katika ngazi ya uchaguzi wa urais .

Mwezi uliopita kulikuwa na malalamiko juu ya kimbunga kinachoweza kusababisha kuwepo kwa mkusanyiko mdogo wa watu.

Zaidi ya dazani mbili za wagombea wanawania kushinda kiti cha uraisi, kilichoachwa na Rais mstaafu Michel Martelly, mwezi February mwaka huu.

Uchaguzi utarudiwa tena endapo hakutakuwa na aliyeshinda zaidi ya nusu ya kura.

Wagombea hao ni Jovenel Moise ambaye ni mfanyabiashara na Martery supporter, Jean Charles ambaye ni mpizani maarufu na Marsye Narcisse anayewakilisha chama cha Rais aliyemaliza muda wake bwana Jean-Bertrand aristide.